Jamii imeshauriwa kutunza mazingira kwa vitendo ikiwa ni pamoja na kupanda miti, kutumia vyoo safi,na kulinda vyanzo vya maji. Hayo ameyasema Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Babati Ndg Salumu Issa leo kwenye maadhimisho ya siku ya Mazingira yaliyofanyika kwa upandaji Miti ktk kitongoji cha Sangara Kijiji cha Sangara Kata ya Riroda H/ Wilaya ya Babati. Kabla ya upandaji miti Wananchi ,Viongozi mbalimbali wa kata ya Riroda wamepewa elimu ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira kuanzia ngazi ya familia ambapo watoa mada kutoka H/ Wilaya ya Babat,RUWASA,na Shirika la WaterAid wameshiriki kutoa Elimu na uhamasishaji wa Wananchi juu ya utunzaji wa Mazingira.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.