Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Lazaro Twange na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Ndg Anna Mbogo Mkoani leo wameshiriki kufanya usafi na kupanda miti na Wananchi wa Kijiji cha Dareda Kati kata ya Ayalagaya Mkoani Manyara ikiwa ni muendelezo wa maandalizi ya maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania.Mara baada ya usafi na kupanda miti, Mhe. Mkuu wa Wilaya Babati amewahamasisha wananchi kuendelea kulinda Amani, kutunza mazingira na kupanda miti na kufanya usafi kila wiki. Wananchi wa kijiji hicho wamehamasika na wamekubaliana katika kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru kila familia ipande miti 10 na ihakikishe inatunzwa.m
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.