Timu ya menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Babati leo imetembelea miradi wa ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ya Manyara Boys. Shule hiyo inayojengwa katika Kijiji cha Ngoley Kata ya Mwada inajengwa na Serikali kupita miradi SEQUIP mpaka kukamilika inategemewa kugharimu kiasi cha Tshs 4.1billion. Timu hiyo imesisitiza mafundi kuongeza nguvu ili mradi huo ukamilike na kuhakikisha wanazingatia viwango vya ubora katika ujenzi wa mradi huo. Shule ya Sekondari Manyara Boys ni shule ya kanda ya kaskazini baada ya kukamilika itapokea vijana kuanzia kidato cha kwanza hadi kidato cha sita.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.