Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mhe.John Noya amepongeza Timu ya Menejimenti kwa usimamizi na ufuatiliaji wa ujenzi wa Miradi ya Maendeleo.Hayo ameyasema leo katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya Babati iliyopo katika Kijiji Cha Mwada wakati Kamati ya fedha Mipango na uongozi ikifanya ukaguzi wa ujenzi wa Wodi ya Wanawake , Wanaume na nyumba ya Kuhifadhi maiti " Tumefurahishwa na kasi ya ujenzi wa majengo hayo, ufuatiliaji wa ununuzi wa vifaa uharakishwe, simamieni mafundi wajenge majengo haya kwa ubora unaotakiwa" amesisitiza kiongozi huyo. Naye Daktari Kiongozi wa H/ Wilaya Dkt Hosea Madama amesema ujenzi uko hatua za lenta ya juu na unategemea kukamilisha mwishoni mwa mwezi mei Mwaka huu.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.