Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Charles Makongoro Nyerere amewapongeza Wananchi wa kata ya Magara na Shirika la Africa Foundation kwa ujenzi wa shule mpya ya Kisasa iitwayo Tara Getty iliyoko Kijiji cha Moyamayoka Kata ya Magara H/ Wilaya ya Babati. Pongezi hizo amezitoa leo shuleni hapo mara baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa shule hiyo kwenye ziara ya Siku ya kwanza kukagua Miradi ya Maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati.
" Wananchi na shirika la Africa Foundation nawapongea sana kwa ujenzi wa shule hii, kinachotakiwa kwa wanafunzi ni kusoma kwa bidii " amesisitiza kiongozi huyo. Shule hiyo inaendelea kujengwa hadi sasa Mfadhili shirika la Africa Foundation ametoa fedha zaidi ya Tsh 295 Million na ujenzi unaendelea.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.