Baraza la Madiwani la H/Wilaya ya Babati limewataka Wadau wa Maendeleo, Mashirika na Idara za Serikali na Halmashauri kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo. Hayo ameyasema M/Kiti wa H/ Wilaya ya Babati Mhe. John Noya leo kwenye Mkutano Maalum wa siku ya Pili wa Baraza hilo wa Kujadili Mpango na Bajeti kwa mwaka 2021/2022 kwa Wadau wa Maendeleo , Mashirika na Idara za serikali uliofanyika Makao Makuu ya H/W -Kijiji cha Loto kata ya Dareda . "Nyinyi Wadau wa Maendeleo, Mashirika na Idara za Serikali na Halmashauri ,wote kwa pamoja tunafanya kazi kuwaendeleza wananchi ni lazima tushirikiane" amesisitiza kiongozi huyo. Katika mkutano huo wajumbe wameliomba shirika la TANESCO kutumia lugha nzuri na kupokea simu wanapopigiwa na Wananchi. Mashirika na Wadau wa Maendeleo waliowasilisha Mipango na Bajeti ni TARURA, RUWASA,TANESCO, NHIF na KARIMU Internationa .Katika kikao hicho wajumbe wamepongeza Wadau wa maendeleo na Mashirika kwa mipango na kazi nzuri wanazozifanya ktk H/W ya Babati
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.