Shule ya Sekondari Manyara Boys imepata heshima kubwa ya kutajwa kuwa shule namba moja kwa ubora wa miundombinu nchini Tanzania ndani ya Mkoa wa Manyara, baada ya kukaguliwa na Makimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa Julai 14, 2025.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, baada ya kukagua mradi huo, alieleza kuridhishwa kwake na ubora wa miundombinu ya shule hiyo, akieleza kuwa ni mfano wa kuigwa kitaifa. Amepongeza jitihada kubwa zilizofanywa na Mkuu wa Wilaya ya Babati, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati na watendaji wote walioshiriki katika kufanikisha ujenzi wa shule hiyo ya kisasa.Katika tukio hilo pia, Mwenge wa Uhuru uliweka jiwe la msingi katika mradi huo uliogharimu kiasi cha shilingi bilioni 4.1, ambapo pamoja na pongezi, wananchi na viongozi wametakiwa kuutunza mradi huo ili uwe na tija kwa vizazi vya sasa na vijavyo.Shule ya Manyara Boys imekuwa chachu ya maendeleo ya elimu katika mkoa huo, na mfano bora wa uwekezaji unaogusa moja kwa moja maisha ya wanafunzi na jamii kwa ujumla
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.