Shule ya Sekondari Mbugwe iliyoko katika Kata Mwada Halmashauri ya Wilaya ya Babati imepandishwa hadhi kuwa kidato cha Tano na sita kuanzia mwaka huu wa fedha wa 2018/2019.Akitoa Taarifa za serikali katika Mkutano wa Baraza la Madiwani Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Ndg. Hamisi Iddi Malinga amesema Serikali imekubali ombi la Halmashauri ya Wilaya ya Babati na kuanzisha kidato cha Tano na sita kwa mkondo mmoja kwa masomo ya CBA na PCB na Halmashauri imeishapokea wanafunzi 80 wa masomo hayo
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.