Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara katika kuhakikisha wanafunzi wote waliofaulu darasani la saba 2018 wanaingia kidato cha kwanza 2019 wamehamasisha wadau na wananchi kukamilisha vyumba vya Madarasa . Akihutubia wananchi na Wadau wa maendeleo, waliojitokeza kwa wingi leo katika kumalizia ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Matufa iliyoko Kijiji cha Matufa kata ya Magugu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Ndg Hamisi Malinga amewashukuru wananchi na Wadau wa Maendeleo waliojitokeza na kusema kukamilika kwa Shule ya Sekondari Matufa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Tawala,pia itasaidia kuwapunguzia umbali watoto waliokuwa wanatembea mwendo mrefu kufuata Elimu katika Shule Mama Sekondari ya Magugu."Mlinituma kufuatilia kibali cha Shule ya Sekondari ya Matufa,napenda kuwajulisha kuwa kibali kimepatikana na wanafunzi wataanza Shule hapa Matufa Wiki ijayo" Amesisitiza kiongozi huyo .Jumla ya wanafunzi 287 Waliokuwa wamebaki wanategemea kuanza Shule hiyo wiki ijayo.Shule ya Sekondari Matufa inajengwa na Wananchi wa Vijiji vitano vya Magugu,Mapea,Sarame,Matufa na Mawemairo .
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.