Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Anna Mbogo amezindua Shule ya msingi mpya ya kifalu juu kwa kuwashukuru wananchi na wafadhili kwa ujenzi wa shule hiyo. Shule ya Msingi kufalu juu iko katika Kitongoji cha Kifalu juu kijiji cha Endakiso Kata ya Endakiso. Mkurugenzi Mbogo ameyasema hayo leo kwenye hafla fupi ya uzinduzi na kuwashukuru wananchi na wafadhili kwa ujenzi wa shule hiyo mpya iliyofanyika katika shule ya msingi Kifalu juu kijiji cha Endakiso Kata ya Endakiso, " Tunawashukuru wananchi na Wafadhili wote walioshirikiana na serikali katika ujenzi wa shule hiyo amesisitiza kiongozi huyo. Wakati huohuo amelishukuru shirika la STC ( So they Can kwa mchango mkubwa katika ujenzi wa shule hiyo lakini kwa ufadhili katika sekta ya Elimu katika kata za Mamire, Endakiso ,Gallapo na Qash. Aidha Mkurugenzi Mbogo ameahidi shule hiyo kusajiliwa haraka ili kutoa huduma katika kijiji hicho
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.