Serikali imetoa fedha kiasi cha Tshs 180,000,000 kukarabati Shule Kongwe ya Msingi ya Gallapo iliyoko kata ya Gallapo H/ Wilaya ya Babati. Akitoa taarifa ya Serikali leo kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani, Uliofanyika Makao Makuu ya H/Wilaya Katibu wa Baraza hilo Mkurugenzi Mtendaji Anna Mbogo amesema Serikali inayoongozwa Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa Robo hii imeleta fedha kiasi cha Tshs 916,000,000 zikiwemo fedha tsh 180 Millioni za ukarabati shule kongwe ya Msingi Gallapo. Naye Diwani wa Kata hiyo Michael Naasi Bim akiwa kwenye mkutano wa Baraza ameshukuru serikali kwa kuleta fedha hizo kukarabati shule hiyo kongwe iliyoanza mwaka 1907. " Sisi wananchi wa kata ya Gallapo hatuna cha kumlipa Mhe. Rais bali tunasema asante sana" amesisitiza Diwani huyo
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.