Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Babati limepongeza Walimu wa shule 5 za sekondari kwa kufanya vizuri katika matokeo ya Mtihani wa Kitaifa wa Kidato cha Sita kwa mwaka 2024. Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa H/Wilaya ya Babati Mhe. John Noya leo katika Baraza la Madiwani lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano. "Tunatambua juhudi kubwa zilizofanywa na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji na Watumishi wa shule zote za sekondari 5 kwa matokeo mazuri ya kidato cha tano hongereni sana" Amesisitiza kiongozi huyo. Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Anna Mbogo amesema anafurahishwa na Matokeo hayo na kutoa pongezi kwa walimu wa shule zote 5 kwa kufahurisha kwa asilimia 100 kwa matokeo ya kidato cha sita kwa mwaka 2024.Shule za sekondari zilizofanya vizuri katika matokeo ya Mtihani wa Kidato cha sita kitaifa na kufahurisha kwa asilimia 100 ni Ayalagaya, Dareda, Mbugwe,Mamire na shule ya Sekondari Chief Dodo .
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.