Serikali inatarajia kujenga shule mpya ya Sekondari katika kata ya Dareda H/ Wilaya ya Babati. Mwenyekiti wa H/ Wilaya ya Babati Mhe. John Noya ameyasema hayo leo kwa nyakati tofauti kukagua maeneo ya ujenzi wa shule hiyo katika vijiji vya Bermi na Seloto akiwa na kamati ya Mipango fedha na uongozi kwenye ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo " Serikali inayoongozwa na Rais Mhe .Dkt Samia inatarajia kutoa fedha kujenga shule mpya katika kata ya Dareda, naomba viongozi na wananchi kutoa ushirikiano mkubwa. amesisitiza kiongozi huyo .Mhe. Noya na kamati yake wamesisitiza viongozi na wananchi kushikamana wakati wote wa utambuzi wa maeneo na wakati wa ujenzi ili mradi huo ujengwe kwa viwango vinavyotakiwa na ukamilike kwa wakati.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.