Wananchi Wilayani Babati Mkoa wa Manyara wametakiwa kutoa ushirikiano nzuri kati yao na wafadhili katika ujenzi wa Miradi ya Maji. Hayo ameyasema Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Eng. Raymond Mushi kwenye Mkutano wa utambulisho wa Mradi mpya wa Maji na Usafi wa mazingira wa Kijiji cha Sangara kata ya Riroda katika Halmashauri ya Wilaya Babati"Wananchi ni lazima watambue miradi hii inayojengwa na serikali kwa kushirikiana na Wadau wa maendeleo ni miradi yao ni lazima wailinde waisimamie na kuiendeleza " amesisitiza Mkuu wa Wilaya. Aidha mkuu wa Wilaya amesisitiza Wananchi kutunza vyanzo vya Maji na mazingira ili kuendelea kunufaika na rasilimali muhimu ya Maji. Mradi wa Maji na Usafi wa Mazingira wa Sangara unafadhiliwa na Shirika la Water Aid na Halmashauri ya Wilaya Babati na unategemea kugharimu kiasi chaTsh 290 millioni mpaka kukamilika kwake.Naye Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la Water Aid Tanzania Ndg Dr. Ibrahim Kabole ameishukuru serikali Wilayani Babati kwa kukubali kupokea Mradi huo na akaomba ushirikiano, katika utekelezaji Mradi huo. Mkutano huo umehudhuriwa na Viongozi wa serikali ya Kijiji, Kata ,H/Wilaya na viongozi kutokaOfisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, taasisi na Mashirika ya UTT, na Shirika la makazi Tanzania ambao wametoa mada mbalimbali juu ya kuulinda, kusimamia na kuendeleza Mradi huo.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.