Wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara wameombwa kusaidia kutoa Elimu ya mapambano dhidi ya Rushwa kwenye jamii wanayoishi nayo ili vitendo vya rushwa vipungue au kutokomea kabisa kwenye jamii.Hayo ameyasema leo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Ndg Hamisi Malinga katika uzinduzi wa Klabu 6 za Wapinga Rushwa za Shule za Msingi na Sekondari kata za Ayalagaya hafla iliyofanyika katika Shule ya Sekondari ya Ayalagaya Kata ya Ayalagaya Tarafa ya Bashnet"Wanafunzi mnauwezo mkubwa wa kuelimisha jamii juu ya mapambano ya Rushwa kupitia Sana'a,na michezo mbalimbali na jamii ikawaelewa na vitendo hivyo vikapungua au kumalizika" Amesisitiza Mkurugenzi Mtendaji huyo.Halmashauri ya Wilaya ya Babati inaendelea kutoa mafunzo na kuunda klabu za Wapinga Rushwa kwa Shule zote za Msingi na Sekondari kwa kushirikiana na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa Mkoa wa Manyara.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.