Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe Queen Sendiga ameagiza viongozi na Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati kukamilisha mapema miradi pendekezwa itakayopitiwa na Mbio za Mwenge Oktoba mwaka huu . Mhe. Sendiga ameyasema hayo leo kwa nyakati tofauti kwenye ziara yake ya ukaguzi wa miradi iliyopendekezwa kupitiwa na Mbio za Mwenge katika Halmashauri ya wilaya ya Babati "Miradi yote iliyopendekezwa ikamilike kwa wakati na iwe na nyaraka muhimu kama ilivyoelezwa kwenye mwongozo wa Mbio za Mwenge 2023" amesisitiza kiongozi huyo. Mhe. Sendinga akiwa kituo cha Afya Bashnet amepongeza Halmashauri ya Wilaya ya Babati , uongozi wa kata na wananchi wa kata ya Bashnet kwa ujenzi wa kituo hicho kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Babati na kusisitiza kazi zinazoendelea zikamilike haraka
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.