Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga amewataka viongozi ngazi zote kutembelea wananchi kuanzia ngazi ya kitongoji kuwasikiliza na kutatua changamoto zao.Mhe. Sendiga ameyasema hayo leo kwa nyakati tofauti kwenye ziara ya kutembelea , kukagua na kusikiliza kero na kuzitatua katika Halmashauri ya wilaya yabBabati katika kata za Mwada,Magugu na Gallapo. Mkuu wa Mkoa akiwa kata za Gallapo na Mwada ameagiza Viongozi wa kata hizo kwenda kufanya vikao na kutatua changamoto zinazowakabili hasa za ardhi na kuwasilisha taarifa ofisi ya Mkuu wa Mkoa"Nendeni mkafanye vikao mkatatue kero zenu mkikubaliana leteni taarifa ofisini kwangu " amesisitiza kiongozi huyo . Aidha Mhe Sendiga amekemea watu wanaochochea migogoro Mkoani Manyara na kusema waache mara moja kwani migogoro haina tija inarudisha nyuma maendeleo ya wananchi.Mhe.Mkuu wa Mkoa akiwa kata ya Magugu amekagua ujenzi wa Shule Msingi Mpya ya Mekiroy inayojengwa kwa fedha za serikali kuu Tsh 348,500,000 kupitia mradi wa Boost na kuagiza taratibu za usajili shule hiyo zianze
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.