Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti amewataka wakazi wa Kijiji cha Vílima Vitatu Kata ya Nkait Halmashauri ya Wilaya ya Babati wanaoishi kwenye Hifadhi ya Wanyama kandokando ya ziwa Manyara kuondoa mara moja ili kuzuia kuenea kwa Ugonjwa hatari wa Kimeta. Hayo ameyasema jana kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Minjingu kata ya Nkait Halmashauri ya Wilaya ya Babati. "Msimamo wa Serikali makazi 17 waliobaki eneo lá hifadhi waondoke mara moja kabla ya kutumia nguvu kubwa, amesisitiza Kiongozi huyo. Kabla ya Mkutano huo Mkuu wa Mkoa, kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya wametembelea eneo lá hifadhi na kujionea ujenzi wa makazi hayo na uharibifu wa mazingira. Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa ameagiza Uongozi wa JUHIBU (Jumuiya ya Hifadhi ya wanyamapori Burunge kutoa kiasi cha Milioni 300 fedha za Kijiji cha Minjingu wanazopata kutokana na uhifadhi kuzipeleka kujenga Kituo cha Afya Nkait.
"Kaa mbali na Shamba lá RIVACU" Haya ni Maneno ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe Alexander Mnyeti akiwataka wananchi wa Kijiji cha Mwada kata ya Mwada kukaa Mbali na Shamba hilo kwani Shamba hilo ni Mali ya Chama cha Ushirika cha RIVACU. Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Mwada kata ya Mwada Halmashauri ya Wilaya ya Babati" Mkitaka kunufaika na Ardhi ya Shamba lá RIVACU jiungeni kwenye Chama chá Ushirika " amesisitiza Mkuu wa Mkoa. Kabla ya Mkutano wa hadhara Mkuu wa Mkoa ametembelea Shamba hilo na kuona wananchi wameanza kulivamia na kuendesha shughuli za kilimo. Shamba la RIVACU limekuwa na mgogoro wa siku nyingi kati ya Chama chá Ushirika cha RIVACU na Wananchi wa Kijiji cha Mwada.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.