Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Alexander Mnyeti amelishukuru Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Babati kwa kusimamia menejimenti vizuri Mpaka Halmashauri hiyo kupata Hati safi. Akizungumza kwenye kikao Maalum cha Mkutano wa Baraza la Madiwani wa H/Wilaya ya Babati leo wakati wa kujadili Taarifa ya Majibu ya Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2018/2019 uliofanyika makao makuu Dareda amesema "Nawapongeza Madiwani kwa kusimamia Menejimenti Vizuri kwa kipindi chote cha Miaka mitano tunawaombea wote mgombee na mchaguliwe tena " Aidha amewaagiza viongozi wa Halmashauri kuanzia ngazi ya Vijiji kutowanyanyasa wananchi bali wawaelimishe, wawaelekeze ,wawaongoze kwenye njia sahihi za kujiletea Maendeleo.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.