Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Queen Sendiga amepongeza wananchi wa Kijiji cha Gidewari kata ya Dabal Halmashauri ya Wilaya ya Babati katika kuchangia Tsh 8,100,00 ujenzi wa madarasa matatu na ofisi moja ktk shule ya Msingi Gidewari . Mkuu wa mkoa ameyasema hayo leo wakati akiweka jiwe la Msingi katika madarasa na ofisi hiyo. Aidha ametumia fursa hiyo kuwashukuru Mamlaka ya Elimu Tanzania ( TEA) kwa kutoa fedha kiasi cha tshs 71,372,640 katika Ujenzi wa madarasa na ofisi hiyo " Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan imelenga kuboresha huduma za elimu na Afya tumuunge mkono" amesisitiza kiongozi huyo. Wakati huo huo Mhe Sendiga amefanya mkutano na wananchi wa kata ya Dabil na kata za jirani ambapo amewasilisha salaam za Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa maeneo hayo. Aidha akiwa katika mkutano huo na wananchi ameagiza maofisa Tarafa, watendaji wa vijiji na kata kutenga siku kuwasikiliza na kutatua kero zao.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.