Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Cuthbert Sendinga ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara kwa kupata Hati safi kwa mwaka wa fedha 2021/2022. Mhe.Sendinga ameyasema hayo leo kwenye Mkutano Maalum wa baraza la madiwani wa kupitia taarifa ya utekelezaji wa hoja za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali( CAG) kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 2022 uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati -Arri "Kupata hati safi ni mipango, taratibu na kufuata sheria na kanuni za fedha hongereni sana kwa kupata hati safi" amesisitiza kiongozi huyo.Mhe. Sendinga ametumia nafasi hiyo kuagiza Halmashauri zote za Mkoa wa Manyara kukamilisha miradi yote ya nyuma mara moja na kusema hataki kuona miradi iliyokaa muda mrefu bila kukamilika.Wakati huo ameagiza maeneo yote ya H/ Wilaya kupimwa na kuwa na hati miliki. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mhe. John Noya ameshukuru,Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya madiwani,Wataalam,Ofisi ya CAG kwa ushirikiano walionesha mpaka kupata hati safi na kuomba ushirikiano huo uendelee
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.