Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Queen Sendiga ameagiza kila mtoto mwenye umri wa kuanza shule apelekwe akaandikishwe kuanzia sasa. Hayo yamesemwa leo kwenye ziara yake kijijini Hoshani kata ya Duru H/ Wilaya ya Babati" Serikali ya Rais Samia inaleta fedha nyingi sekta ya ya Elimu hivyo kila mtoto mwenye umri wa kuandikishwa shule akaandikishwe na mwezi januari 2024 apelekwe shule" amesisitiza kiongozi huyo.Mhe. Sendiga akiwa kijiji cha Endadment kata Gidas amekagua ujenzi wa mradi wa kituo cha Afya Gidas na ameongea na wananchi na kusikiliza kero za wananchi ambapo ameagiza Meneja wa RUWASA kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha maji yanatoka katika kata hiyo. Wakati huo huo amepiga marufuku kwa walimu kurudisha watoto nyumbani kwa kukosa michango ambayo wamekubaliana kwenye mikutano. Naye Mbunge wa Babati Vijijini Mhe . Daniel Sillo ameshukuru Serikali kwa kutoa fedha nyingi katika sekta ya Afya, Elimu na Maji.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.