Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suhulu Hassani anategemea kufanya ziara ya Kikazi Mkoani Manyara kuanzia tarehe 22 Hadi 23/11/ 2022 . Akizungumza leo na Viongozi wa Kata, serikali za vijiji na Mitaa na wataalamu mbalimbali kwa nyakati tofauti kwenye ukumbi wa jengo la H/ Wilaya ya Babati, ukumbi wa CCM Mkoa , Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe Lazaro Twange amesema" Nimeona niwaite Viongozi wote Wilaya ya Babati na kuwaeleza ujio wa Mhe . Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mkoani Manyara hususani Wilaya ya Babati kuanzia trh 22 Hadi trh 23/11/2022" amesisitiza kiongozi huyo.Katika maelekezo yake amesisitiza Viongozi hao kwenda kuwaeleza Wananchi wote ujio wa Mhesimiwa Rais na wajitokeze kwa wingi kumpokea na kumsikiliza atakapokuwa anahutubia Wananchi kwenye uwanja wa Kwaraa mjini Babati trh 22/11/2022 kuanzia saa 3.00 asubuhi . Aidha amesisitiza Wananchi wote kutoka maeneo yote wahudhurie bila kukosa kumpokea na kumsikiliza Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.