Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe Elizabeth Kitundu amewashukuru Viongozi,Wananchi na Wawekezaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati kwa kuchangia fedha na Vifaa mpaka kukamilisha vyumba vya Madarasa na kuwezesha Wanafunzi waliofaulu mtihani wa darasa la saba 2018 kuanza masomo ya kidato cha kwanza 2019. Hayo ameyasema Leo kwenye Kikao cha pili cha Mkutano wa Baraza laMadiwani uliofanyika leo katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati "Nawashukuru sana Madiwani, wananchi Watumishi,Viongozi na Wawekezaji kwa michango na vifaa mbalimbali vilivyowezesha kukamilisha madarasa. Naomba ushirikiano huo uendelee" Amesisitiza Mkuu wa Wilaya. Aidha Mkuu wa Wilaya ameagiza Mkurugenzi Mtendaji kuwachukulia hatua watumishi ambao hawatekelezi majukumu yao ipasavyo na kupelekea shughuli nyingi kukwama.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.