Kamati ya fedha, Mipango na uongozi ya H/ Wilaya ya Babati imeagiza kamati ya Maendeleo ya Kata ya Qash kukaa na kuangalia upya ujenzi wa Shule mpya ya tatu inayojengwa na kamati ya Maendeleo ya Kata hiyo. Hayo yamesemwa leo na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe.Yahaya Loya wakati kamati ya fedha , Uongozi na mipango wakiwa kwenye ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo. " Tumekagua maendeleo ya ujenzi wa Shule mpya Ktk Kata yenu,tunaagiza nendeni mkae upya na kubainisha ni vijiji vipi vinachangia ujenzi wa Shule mpya" amesisitiza kiongozi huyo. Akisoma taarifa Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Shule hiyo Ndg Pius Vanjenja amesema kusimama Kwa ujenzi wa Shule hiyo ni kutokana na ushiriki hafifu wa utoaji michango Kwa baadhi ya vijiji vya Kata hiyo.Mpaka Sasa Kata ya Qash inazo Shule za Sekondari 2 ambazo ni Qash, Organdida na inajenga Shule mpya ya 3 inayojengwa Kijiji cha Majengo kwa Sasa wameanza na vyumba Viwili vya Madarasa na ofisi moja vyote viko hatua ya Msingi.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.