Mwenyekiti wa H/ Wilaya ya Babati Mhe John Noya amepongeza shirika la Karim Foundation kwa kushirikiana na H/Wilaya Babati na wananchi wa kijiji cha Dohom kwa ujenzi wa matundu ya vyoo 28 katika shule ya Sekondari Dohom iliyoko kata ya Arri.Mhe. Noya ameyasema hayo leo kwenye hafla fupi ya kuweka jiwe la ufunguzi wa ujenzi wa mradi huo iliyofanyika leo shule ya Sekondari Dohom" Tunashukuru serikali ya Awamu ya Sita kwa kushirikiana na Karim Foundation ,wananchi katika ujenzi wa matundu 28 ya vyoo katika shule hii ushirikiano huo uendelee" amesisitiza kiongozi huyo.Katika hotuba yake amesisitiza utunzaji wa mradi kwa manufaa ya wengine na akaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa Serikali inayoongozwa na Rais Mhe Dk Samia Suluhu Hassan. Wananchi wa kijiji cha Dohom wameshukuru Serikali na Mfadhili Karim Foundation na kuahidi kutoa ushirikiano kwa miradi mingine inayojengwa na serikali na wafadhili.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.