Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mhe. John Noya ameshukuru Serikali kwa kutoa fedha kiasi Cha Tsh 230,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa Majosho 10 katika Vijiji vya Halmashauri Wilaya ya Babati. Mhe Noya ameyasema hayo leo katika Kijiji Cha Kakoi Kata ya Nkait wakati Kamati ya Ujenzi , Uchumi na Mazingira ikikagua miradi ya Maendeleo robo ya Tatu ya Mwaka huu " Tunashukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kutoa fedha kujenga Majosho katika Vijiji vyetu, hii itasaidia kuboresha mifugo na mazao yatokanayo na mifugo na kuongeza kipato kwa wafugaji na jamii Kwa ujumla" amesisitiza kiongozi huyo. Mwenyekiti huyo amesisitiza mkandarasi anayejenga Majosho hayo kukamilisha kwa wakati na Wananchi kutunza Majosho hayo baada ya kukamilika. Wizara ya Mifugo na Uvuvi imetoa fedha Kiasi Cha Tsh 230 Million kwa ajili ya ujenzi wa Majosho 10 katika Vijiji. 10 vya H/ Wilaya ya Babati na Majosho hayo yanaendelea na ujenzi na yako katika hatua mbalimbali za ukamilishaji
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.