Mwenyekiti wa H/ Wilaya ya Babati Mhe. John Noya amepongeza Shirika la So they Can Tanzania STC kwa kushirikiana na wananchi wa Kitongoji cha Kifaru juu kijiji cha Endakiso kata ya Endakiso Kujenga shule mpya ya Msingi. Mhe. Noya ameyasema hayo leo kwenye ukaguzi wa miradi na kamati ya Mipango , fedha na Uongozi ikiwa kata ya Endakiso " Kwa niaba ya Baraza la Madiwani Tunawashukuru So they Can na Wananchi kwa ujenzi wa shule hiyo" amesisitiza kiongozi huyo.Aidha Mhe. Noya amewaomba Uongozi wa So They Can na wananchi kwa Kata yaEndakiso kuendelea kushirikiana kujenga nyumba ya Mwalimu na vyoo ili shule hiyo iweze kufunguliwa mapema.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.