Mwenge wa Uhuru umeweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Kituo cha Afya Gallapo kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati, Mkoa wa Manyara.Tukio hilo limeongozwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ndugu Ismail Ali Ussi, ambapo ameeleza kuwa ujenzi wa kituo hicho ni ushahidi wa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha huduma za afya hadi ngazi ya jamii.Kituo hicho cha afya kinatarajiwa kuhudumia maelfu ya wananchi wa Kata ya Gallapo na maeneo ya jirani, kikiwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi waliokuwa wakisafiri umbali mrefu kufuata huduma za matibabu.Katika hotuba ya uzinduzi, wananchi wamepongeza jitihada za Serikali na kuahidi kushirikiana kwa karibu kulinda miundombinu hiyo na kuhakikisha kituo kinatumika kwa tija. Viongozi wa Serikali kwa upande wao wamehimiza usimamizi thabiti wa mradi huo hadi kukamilika kwa viwango vinavyotakiwa.Kuwekwa kwa jiwe hilo la msingi ni sehemu ya miradi inayotembelewa na Mwenge wa Uhuru 2025 katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati, ikiwa ni ishara ya kusherehekea mafanikio ya maendeleo nchini.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.