Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Eng Raymond Mushi amewataka Watendaji wa kata, Maofisa Elimu Kata na Watendaji wa Vijiji kusimamia kikamilifu ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule za Msingi na Sekondari katika maeneo yao. Hayo ameyasema leo kwenye kikao Maalum cha Watendaji hao kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati "Tunataka shule zetu zote ziwe na matundu ya vyoo vya kutosha na vijengwe na Wananchi na Wahisani wengine na kazi hii imalizike mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu" Mkuu wa Wilaya amesisitiza. Aidha amewataka Watendaji hao kusimamia ujenzi wa matundu kujengwa kwa kiwango kinachotakiwa na Ukaguzi kwa kila shule utaanza mwishoni mwa mwezi Julai .Mkuu wa Wilaya amesema kuna Magonjwa mengi yanayowapata wanafunzi wakiwa Shuleni hivyo ni lazima tuweke mkakati wa ujenzi wa matundu ya vyoo kwa kila shule kwani ni muhimu Sana katika maendeleo ya jamii. Mtendaji wa Kijiji cha Hallu kata Gallapo Halmashauri ya Wilaya ya Babati Ndg January Cosmas Doita kwa niaba ya Wajumbe wa kikao hicho amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kuweka mkakati huo kwani ukosefu wa matundu ya vyoo katika shule za Msingi na Sekondari ni tatizo kwenye baadhi ya kata na vijiji na kuahidi kwenda kuanza utekelezaji wa ujenzi wa matundu ya vyoo.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.