Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Elizabeth Kitundu amepongeza Halmsahauri ya Wilaya ya Babati kwa ukusanyaji mapato ya ndani kwa mwaka 2019/2020 na kufikia asilimia 90 mpaka sasa na kusisitiza kuongeza bidii mpaka kufikisha asilimia 100 ifikapo Juni 30,2020. Hayo ameyasema leo kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani la H/Wilaya ya Babati lillilofanyika katika Makao makuu Kata ya Dareda."Halmashauri mnatakiwa kuongeza bidii kukusanya mapato yote ili kuweza kukamilisha miradi ya maendeleo iliyopangwa" Amesisitiza Kiongozi huyo.Aidha amesisitiza matumizi ya fedha zote yafuate taratibu kanuni na sheria za matumizi ya fedha za serikali.Wakati huo huo amesisitiza wananchi Kuhifadhi chakula kinachovunwa katika msimu huu ili kuweza kuweka usalama wa Chakula
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.