Mkuu wa Wilaya ya Babati amewashukuru Vijana wanaoshiriki mafunzo ya Jeshi lá akiba .Mkuu huyo ameyasema hayo katika ufunguzi wa Mafunzo ya jeshi lá akiba yanafanyika Kiwilaya Kata ya Kisangaji Kijiji cha Kisangaji Katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati. Aidha amesisitiza Vijana hao kushiriki katika Kazi za maendeleo ili kujiletea maendeleo. Kabla ya Ufunguzi huo Mkuu wa Wilaya ameongea na Kamati za Maendeleo za kata za Magugu, Mwada na kisangaji. Mkuu wa Wilaya Pia ameongozana na wajumbe Kamati za ulinzi na usalama ambao wametoa Ujumbe na ufafanuzi wa mambo mbalimbali.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.