Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Lazaro Twange ameongoza taasisi mbalimbali kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa. Mhe. Twange amefanya hivyo ikiwa ni utekelezaji wa kliniki ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi iliyofunguliwa leo na Ndg Paul Makonda Katibu wa Halmmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi , uenezi na Mafunzo katika Viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Manyara. Ndg Makonda jana kwenye Mkutano wa hadhara katika viwanja vya Stendi Babati mjini aliagiza taasisi zote za serikali kwenda viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara kusikilza na kutatua kero za wananchi. Wakati akiendelea kusikiliza kero za wananchi Mhe, Twange amewaambia wananchi kuwa ofisi yake iko wazi kila siku wananchi wasisite kufika kutatuliwa kero zao na wengine amewaahidi kuwafuata katika vitongoji vyao wanakoishi ili kuhakikisha kero zao zinatatuliwa. Katika viwanja hivyo wananchi kutoka wilaya ya Babati na wilaya nyingine wamejitokeza kwa wingi kutatuliwa kero zao.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.