Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati ndugu Hamisi Iddi Malinga akiongozana na Mganga Mkuu wa Wilaya na Wataalamu wengine wa Afya wameamua kutoa Elimu juu ya ugonjwa wa Mlipuko Corona ulioripotiwa kuathiri nchi mbalimbali duniani.Mkurugenzi huyo ameamua kufanya ziara hiyo katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya babati kutoa Elimu hiyo baada ya ugonjwa huu kuripotiwa kuenea katika maeneo mbalimbali Tanzania,” Visa mbalimbali vimeweza kuripotiwa hii ikiashiria ugonjwa huu tayari upo nchini”ameeleza Mkurugenzi huyo na kuwaomba wananchi kufuata maelezo na miungozo mbalimbali inayotolewa na wizara ya Afya na wataalamu wengine wa afya nchini, nae Mganga Mkuu wa Wilaya Dk Madama Hosea amewatahadharisha wananchi pindi wanaposikia dalili za ugonjwa wa corona ikiwa ni pamoja na kupanda kwa joto mwilini, kupata kikohozi kikavu, viungo vya mwili kuuma na mwili kuishiwa nguvu, kupata mafua makali yanayoambatana na homa kali kufika haraka katika kituo cha afya, zahanati au hospitali kwa ajili ya uchunguzi, ameeleza ugonjwa huu huambukuza kwa njia ya matone ya majimaji yanayotoka katika mwili wa mtu ambaye tayari ameshaambukizwa na ugonjwa huu ikiwa ni pamoja na mate au mafua mtu anapopiga chafya hivyo amewasisitiza wananchi kufunika kinywa pindi unapopiga chafya na pia kunawa mikono na maji yanayotiririka na sabuni kuepuka kupata maambukizi haya ya ugonjwa hatari wa Corona.”mpaka sasa hakuna kisa kilichoriporiwa katika Mkoa wa Manyara wala katika wilaya yetu ya Babati ila tufuate kanuni za afya ili tuendelee kubaki salama” amesisistiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Babati
Mganga mkuu wa Wilaya akieleza namna ya kujikinga na Ugonjwa wa Corona
Baadhi ya sabuni za kunawia Mikono
ndoo zenye maji yanayotiririka
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.