Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Babati Anna Mbogo amewaomba Wah.Madiwani kuhamasisha wananchi katika maeneo yao wajitokeze kwa wingi katika zoezi la uboreshaji kwenye Daftari la kudumu la wapiga kura.Mkurugenzi mtendaji ameyasema hayo leo kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani lililofanyika leo katika ukumbi wa Mikutano. "Wahe.Madiwani zoezi la uboreshaji Daftari la kudumu la Wapiga kura katika Halmashauri yetu litafanyika kwa siku 7kuanzia tarehe 04 hadi tarehe 10/9/2024 hivyo tuhamasishe wananchi wajitokeze kwa wingi katika vituo 228 vilivyoko vijijini kuboresha taarifa zao kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2025.Wakati huo huo amesema zoezi hilo litahusisha kuandikisha wapiga kura wapya raia wa Tanzania waliotimiza miaka 18 na kuendelea, waliohama eneo moja la uchaguzi kwenda lingine,ambao taarifa zao zilikosewa wakati wa kujiandikisha aliyepoteza kadi au kadi yake kuharibika na waliopoteza sifa la kuwemo kwenye daftari la kudumu la wapiga kura mfano waliofariki hivyo kuwaomba wajitokeze
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.