Mkurugenzi Mtendaji Anna Mbogo amepongeza uongozi wa Kiwanda cha Itracom Fertilizer LTD kwa ujenzi wa kiwanda hicho katika Kijiji Vilima vitatu kata ya Nkait H/ Wilaya ya Babati." Mkurugenzi Mbogo ameyasema hayo leo wakati Timu ya Menejimenti ya H/Wilaya ya Babati ikikagua na kufuatilia miradi ya Maendeleo vijijini "Tunawapongeza sana Uongozi wa kiwanda kwa ujenzi wa kiwanda hiki kwani kitaongeza mapato na Ajira katika Halmashauri yetu".Kiwanda cha Itracom kinahusika na uchakataji wa malighafi za kutengeneza mbolea. Naye Meneja wa Uzalishaji Ndg Ipyana Mwandete amepongeza uongozi wa H/ Wilaya Babati kwa ushirikiano mkubwa tangu wanaanza mpaka kufikia hatua hiyo.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.