Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Ndg Hamisi Malinga ameutaka uongozi wa Jumuiya ya Wanyamapori Burunge(JUHIBU) kutumia vizuri fedha wanazozipata katika kuleta maendeleo ya Wananchi walioko kwenye Jumuiya hiyo.Hayo ameyasema Leo kwenye Hafla fupi ya kuwaapisha wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Jumuiya hiyo iliyofanyika ofisini kwao Kijiji cha Mwada Kata Mwada. "Asitokee mtu yeyote akapewa fedha bila utaratibu,fedha hizo tutakudai" amesisitiza Mkurugenzi Mtendaji.Katika hafla hiyo amewasisitiza Viongozi waliopishwa kusimamia Mali za Jumuiya na kuhakikisha fedha zote kabla hazijatumika zipelekwe Bank na Fedha hizo zitakaguliwa kila mara. Naye Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Magugu Mh.Christina Kisamo amewataka Wajumbe wa Bodi hiyo kuheshimu kiapo chao na wafanye kazi kwa makini na uadilifu na kwa kuzingatia sheria za nchi.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.