Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi DKt Zakia Mohammed Abubakari amewapongeza wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati kwa kuendelea kujitokeza kuhakiki na kuboresha taarifa zao kwenye zoezi la Uboreshaji Daftari la kudumu la Wapiga kura. Dkt Zakia ameyasema hayo leo wakati alipotembelea vituo kwenye kata za Magugu, Mwada na Nkait na kujionea jinsi zoezi linavyoendelea. Akiwa katika Kituo Cha Ofisi ya Kata Mwada amejionea jinsi wananchi wanavyohakiki majina yao yaliyobandikwa na na kuwaomba kwenda kuwa Wajumbe wazuri kuwaelimisha wengine" Nawapongeza sana wananchi nendeni mkawe Wajumbe wazuri kuelimisha wengine nao waje" amesisitiza kiongozi huyo. Kwa Upande wake Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Babati Vijijini Anna Mbogo ameshukuru Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kwa kutembelea Jimbo la Babati Vijijini na kuhaidi maelekezo yote yanayotolewa yatatekelezwa kwa wakati
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.