Mkurugenzi Mtendaji wa H/Wilaya ya Babati Anna Mbogo amejiwekea utaratibu wa kufuatilia na kukagua miradi ya ujenzi sekta ya Elimu na Afya ili miradi hiyo ijengwe kwa ubora unaotakiwa na ikamilike kwa wakati .Akikagua ujenzi wa madarasa 8 ya Shule ya Msingi Vilima , Mkurugenzi Mtendaji amesisitiza ujenzi huo ufuate viwango vya ubora vinavyotakiwa na amesisitiza kila hatua wanayofikia ni lazima ikaguliwe na mhandisi wa ujenzi ili kujiridhisha na ubora wa jengo, akiwa kituo Cha Afya Gidas kinachojengwa na serikali ,Mkurugenzi Mtendaji, amekutana na kamati za ujenzi na kusisitiza wajumbe kusimamia kwa umakini ujenzi wa kituo hicho pia ameshiriki na Wananchi Ktk ujenzi wa msingi wa majengo ya OPD na Maabara ktk kituo hicho.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.