Halmashauri ya Wilaya ya Babati inategemea kusajili ngombe 200,000 Kwa kutumia hereni za kielektroniki. Afisa Mifugo na Uvuvi Ndg Gilbert Mbesere amesema hayo leo Ktk Kijiji cha Ngoley Kata ya Mwada akiwa anaendelea na zoezi la usajili. Zoezi hilo limezinduliwa na Mh. DC tarehe 29/09/2022. Mpaka sasa jumla ya ng'ombe 1,025, Mbuzi 1,270, Kondoo 583 na Punda 03 wamesajiliwa.
Ndg Mbesere amewasisitiza wafugaji wote kuhakikisha wanapeleka Mifugo yao kusajiliwa. Kwa kufanya hivyo kutarahisisha ufuatiliaji wa matukio kama wizi, magonjwa ya Mifugo na masoko ya ndani na nje kwa wafugaji. Aidha akiwa Kata ya Mwada vijiji Ngoley na Mwanda amewaomba wenyeviti wa vijiji na Vitongoji kuhamasisha wafugaji kusajili Mifugo yao kuanzia wenye umri wa miezi 3 na kuendelea kwani zoezi hilo lina umuhimu mkubwa kwa jamii na taifa Kwa ujumla.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.