Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Charles Makongoro Nyerere amewashukuru Wananchi wa Mkoa wa Manyara kwa kupanda miti na kufanya usafi maeneo mbalimbali katika kuelekea Maadhimisho ya kilele cha Miaka 59 ya Muungano. Mhe Makongoro ameyasema hayo leo kwenye kilele Cha Maadhimisho ya Miaka 59 ya Muungano iliyofanyika kimkoa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Kata ya Gallapo katika Kijiji Cha Gallapo Uwanja wa Mpira."Nawashukuru Wananchi katika Wilaya zote kwa kufanya usafi ,kupanda miti katika kuelekea kilele Cha Miaka 59 ya Muungano " amesisitiza kiongozi huyo. Mhe. Makongoro ametanabaisha kuwa ili kuendelea kuuenzi Muungano Wananchi wanatakiwa kuendelea kulinda amani iliyopo nchini, kufanya kazi kwa bidii,kutunza vyanzo vya Maji,kupanda miti na kuitunza. Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa ametumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kutekeleza miradi ya Maendeleo katika Mkoa wa Manyara .
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.