Miradi mingi ya maji kujengwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara.Akizungumza leo ofsini kwake Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini Wilayani Babati (RUWASA) Felix Mollel amesema anashukuru serikali inayoongozwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kujenga miradi ya maji Wilayani Babati. Ndg Mollel ametaja baadhi ya miradi itekelezwa na ofisi yake kwa upande wa H/ Wilaya ya Babati kuwa ni Mradi wa Maji Kazaroho ( umepewa Tsh 648 Million), mradi wa maji Vilima Vitatu umepewa Tsh 1.3 Billion) , mradi wa maji Madunga umepewa Tsh 3.5 Billion na mradi wa Maji Boay, Hoshani na Magara umepewa Tsh 1.8 Billion) kwa kutaja michache. Amesema miradi hiyo iko hatua mbalimbali za utekelezaji. Wakati huohuo Ndg Mollel ameomba viongozi na wananchi mahali kote miradi hiyo inakotekelezwa kutoa ushirikiano mkubwa wakati wote wa utekelezaji miradi ya maji ili kila mwananchi aweze kupata maji bombani kwa wakati.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.