Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Manyara Mhe. Regina Ndege amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Babati kwa mapambano ya Ukatili wa kijinsia katika Wilaya ya Babati. Mhe. Ndege ameyasema hayo leo kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani la H/ Wilaya Babati lililofanyika leo kwenye ukumbi wa Mikutano." Mhe Mkuu wa wilaya tunakupongeza kwa juhudi zako za kupambana na ukatili wa kijinsia tunaomba jitihada hizo ziendelee" amesisitiza kiongozi huyo.Kwa mara nyingine tena Mhe. Ndege amesisitiza madiwani kwenda katika maeneo yao kupambana na pombe aina ya gongo ili kuokoa vijana kwani pombe hiyo inamaliza nguvu kazi katika maeneo ya vijijini
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.