Watumishi wa Idara ya Afya na Elimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati wametakiwa kusimamia vyema na kwa weledi zoezi la umezeshaji dawa za Minyoo ya Tumbo katika shule za Msingi.Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Babati ndugu Hamis Idd Malinga katika kikao cha utekelezaji wa agizo hilo katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Babati kati ya Maafisa Elimu,Maafisa Afya pamoja na Warataibu wa zoezi la umezeshaji wa dawa za Minyoo Tumbo.
”Tumieni Elimu, Uzoefu na Weledi kuhakikisha zoezi la umezeshaji dawa za Minyoo Tumbo kwa wanafunzi wa shule za Msingi linafanikiwa kwa kiwango kikubwa” Amesisitiza Mkurugenzi Mtendaji, Aidha amesema kufanikiwa kwa zoezi hilo kutafanya watoto wakue vizuri na kukuza uwezo wa ufahamu na uelewa shuleni.
Naye Mratibu wa zoezi hilo ndugu James Mleli amesema zoezi hilo litaanza kwa uhamasishaji kuanzia ngazi za vitongoji,vijiji na shule ili kuwapa jamii uelewa na umuhimu wa kumeza dawa hizo.Umezeshaji dawa za Minyoo Tumbo katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati linategemea kufanyika tarehe 19/4/2018 kwa shule za Msingi 143 zenye wanafunzi 84,354 wenye umri kati ya miaka 5 hadi 7.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.