Halmashauri ya Wilaya ya Babati imeanza kutoa chanjo ya mifugo Ili kuzua magojnjwa ya mifugo. Akikabidhi chanjo ya kuku leo katika viwanja vya H/Wilaya ya Babati iitwayo Tatu Moja kwa Maofisa ugani kwa ajili ya kutibu magojnwa ya Kideri,Ndui, na Mafua makali ya Kuku , Ndg Benedict Ntabagi kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa H/ Wilaya Babati amewaeleza maofisa ugani hao kwenda kutoa chanjo hiyo kwa wafugaji wote kwa weledi wa hali ya juu Ili kuzuia magonjwa hayo. Naye Afisa Mifugo wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Ndg Patrick Kisamo amesema chanjo hiyo imetolewa na Serikali kupitia Wizara Mifugo na akatumia fursa hiyo kwa niaba ya wafugaji kuishukuru Serikali inayoongozwa na Dkt Mhe Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa chanjo hiyo wakati huu ambao mahitaji ya chanjo hiyo ni makubwa. Chanjo ya Tatu Moja imeanza kutolewa leo na itatolewa katika vijiji vyote 102 vya Halmashauri ya Wilaya ya Babati na chanjo za Mifugo mingine zitaendelea kutolewa
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.