Maofisa Elimu Kata wametakiwa kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha wanasimamia taaluma katika maeneo yao ili kuinua kiwango cha Elimu. Hayo ameyasema Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini Mhe. Jitu Soni wakati wa kukabidhi pikipiki 25 Kwa Maofisa Elimu kata 25 wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati leo katika viwanja vya Ofisi za Makao mkuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Babati. "Tumieni pikipiki hizo kwa vitendo kurahisisha shughuli zenu za kuinua kiwango cha taaluma katika maeneo yenu" amesisitiza Mhe. Mbunge. Akisoma maelekezo yaliotolewa na Serikali Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Ndg. Hamisi Iddi Malinga amesisitiza Maofisa hao kuzitunza pikipiki hizo,na kuhakikisha zinafanya kazi iliyokusudiwa na kuwaeleza kuwa kila mmoja atajaza Mkataba kulingana na mwongozo wa pikipiki hizo. Naye Mwenyekiti wa Maofisa Elimu Ndg. Peter Yaghambe Kwa niaba ya Maofisa Elimu kata wote ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutekeleza ahadi yake ya kuwapatia vitendea kazi kwani ilikuwa kilio chao cha Muda mrefu .Pikipiki hizo zimetolewa na serikali kwa kushirikiana Wadau Elimu mbalimbali katika Programu ya Equip-T na LANES na Halmashauri ya Wilaya Babati imepata pikipiki hizo kwa asilimia 100.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.