Maofisa Elimu kata wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati wamepatiwa Pikipiki kwa ajili ya kusaidia kutekeleza majukumu yao. Akitoa taarifa za Serikali kwenye Mkutano wa Baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Babati unaofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Ndg. Hamisi Malinga amesema Serikali kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali wa Elimu hasa kupitia Programu za Equip-T na LANES imenunua pikipiki 25 kwa Maofisa Elimu hao ili kuongea ufanisi wa utendaji Kazi.Wajumbewamepongeza serikali na kusema Maofisa hao wapewe pikipiki hizo kwa kusaini mkataba na Ofisa akihamishwa au kustaafu akabidhi pikipiki hiyo Halmashauri ya Wilaya ya Babati.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.