Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati wameshauliwa kushirikiana na watumishi kukusanya mapato ya ndani kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu na kutoa huduma bora kwa Wananchi. Hayo ameyasema Makamu Meya wa Manispaa ya Kahama Mhe. Sindano Machum leo wakati wa ziara ya Wahe Madiwani wa H/ Wilaya ya Babati walipotembelea Manispaa ya Kahama kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo ukusanyaji wa Mapato ya ndani,uwezeshaji wa Wananchi kiuchumi, usimamizi wa Miradi hususani miradi ya mapato ya ndani."wakati mwingine sisi Madiwani tunakwamisha ukusanyaji mapato ya Halmashauri, Watumishi wanapokuja kukusanya mapato ya leseni sisi tunatoa taarifa kwa Wananchi wafunge maduka, Nawashauri nyinyi Madiwani msifanye hivyo" amesisitiza kiongozi huyo, naye Mwenyekiti wa H/ Wilaya ya Babati Mhe. John Noya amesema yote mazuri waliojifunza Manispaa ya Kahama wataenda kuyafanyia kazi Kwa haraka ili yalete tija Kwa wananchi na Serikali Kwa ujumla
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.