Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Anna Mbogo amewaomba Madiwani kutumia na kusambaza matokeo ya sensa ya mwaka 2022 katika kupanga mipango ya maendeleo ya kata. Mkurugenzi huyo ameyasema hayo leo kwenye mkutano wa Baraza la madiwani lililofanyika leo kati Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati. "Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kushirikiana na Ofisi yangu imetoa matokeo ya Idadi ya watu na idadi kaya katika kata 25 za Halmashauri ya Wilaya ya Babati ,kwa sensa ya mwaka 2022 Halmashauri ya Wilaya ya Babati ina watu 375,200 ambapo wanaume ni 192,091 na wanawake 183,109 na Idadi ya Kaya ni 80,578" amesisitiza kiongozi huyo. Wakati huo ameomba wahe. Madiwani kuhamasisha na kuelimisha wananchi kutumia matokeo ya sensa 2022 katika mipango ya shughuli mbalimbali za maendeleo katika kata.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.