Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Babati limepongeza Serikali Kuu kwa kuipatia fedha kiasi cha bilioni mbili kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Utawala Makao Makuu na Ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Babati. Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Baraza hilo Mhe. John Noya katika Mkutano wa Baraza hilo uliofanyika leo Makao makuu ya H/Wilaya Dareda. "Tunaishukuru Serikali kwa kutupatia kiasi cha Bilioni 1 ujenzi wa jengo la Utawala na Bilioni 1 Ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Babati"Mwenyekiti huyo amesema ujenzi wa jengo la Utawala Makao makuu umeanza na unaendelea vizuri ktk Kijiji cha Endasago Kata ya Arri na ujenzi wa Hospitali ya H/Wilaya awamu ya pili unaendelea vizuri ktk Kijiji cha Mwada Kata ya Mwada.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.